Sionelei kuwa inajuzu kuingia katika bunge pasi na kujali anayesema kitu kigine. Kuingia katika bunge maana yake ni kukubali matokeo hata kama itakuwa hukumu ya Twaaghuut. Ikiwa unajua tangu hapo mwanzo kwamba umelazimika kukubali matokeo haya, basi wewe uko katika hali ya khatari. Bunge maana yake ni watu ndio wanaongoza ingawa mwandishi wa ”As-ilat-uth-Thawrah” alimelisapoti. Katika kitabu hichi amepotea sana. Soma Radd mbili dhidi ya mwandishi wa ”As-ilat-uth-Thawrah”. Zimechapishwa na himdi zote ni Zake Allaah. Moja wapo imeandiwka na ndugu yetu na muheshimiwa Shaykh ´Aliy bin Ahmad Abaa Butayn na nyingine inaitwa “Jinaayatu As-ilat-ith-Thawrah ´alaal-Islaam” ya muheshimiwa Shaykh na Dr. Fahd al-Fuhayd.

Kitabu hichi kinachoitwa “As-ilat-ith-Thawrah” mwandishi anaita katika wakati wa washirikina wa mwanzo. Mwandishi wake anaita kikamilifu katika wakati wa washirikina wa mwanzo. Ameenda hata kinyume na uongozi wa Makhaliyfah waongofu. Amekubali raia kuongoza na kujuzisha raia kutunga hukumu zao pasi na kurejea katika Shari´ah. Hii ni fedheha kwa watu kama hawa na tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=144446
  • Imechapishwa: 23/04/2015