Swali: Ni vipi mume anamsusa mke?

Jibu: Kama ilivyopokelewa:

”… na wala asimuhame isipokuwa nyumbani.”

Mke akimtii basi inatosha. Huku ndio kususa. Akimsusa kwa maneno iwe kwa muda wa siku tatu. Hivi ndio kususa. Asizidishe siku tatu kutomzungumzisha. Kususa kwa maneno inakuwa kwa muda wa siku tatu na chini ya hapo. Kuhusu kumsusa kimatendo ni kwa njia ya kumpa mgong au kumuonyesha kumkasirikia kwake mpaka ashike adabu juu ya yale anayoenda kinyume. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahama baadhi ya wakeze mwezi mmoja na akajitenga nao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21645/كيف-يكون-هجر-الزوج-لزوجته
  • Imechapishwa: 01/09/2022