Kutamani mgonjwa aliyeugua kipindi kirefu afe

Swali: Kuna mtu alikuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu kisha akafa. Wakasema ´imekuwa vizuri vile amekufa`. Je, kuna ubaya wa kusema hivo?

Jibu: Haitakikani kusema hivo. Allaah ndiye anajua uhakika. Pengine ilikuwa vizuri kwake endapo angeendelea kuishi. Mgonjwa kila ambavyo unaendelea ugonjwa wake ndivo zinavyoongezeka thawabu zake na kusamehewa madhambi yake. Kila ambavyo yanaongezeka masiku ya kuugua kwake ndivo Allaah anamsamehe makosa yake:

”Mja hapatwi na kutaabika, uzito, maradhi, huzuni, maudhi, dhiki mpaka ule mwiba unaomchoma isipokuwa Allaah humfutia dhambi zake kwayo kama ambavo majani yanavopukuchika kwenye mti.””

”Watu wenye majaribio makubwa ni Manabii, kisha waja wema, kisha wanaofanana nao na wanaofanana nao.”

Swali: Mtu amepatwa na maradhi kwa kipindi kirefu na baadhi yao wanatamani afe na kufikia kusema kuwa endapo angekufa ingekuwa ni kheri kwake.

Jibu: Yote haya ni makosa. Haitakikani hivo. Allaah anamfutia makosa kutokana na maradhi yaliyompata. Mola Wako ni mwingi wa hekima, Mjuzi wa kila kitu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21637/حكم-استحسان-الموت-لمن-طال-مرضه
  • Imechapishwa: 01/09/2022