Namna ya kuyatolea Zakaah mapambo ya dhahabu

Swali: Nimesikia kuwa mwanamke analazimika kuyatolea zakaah mapambo yake ya dhahabu hata kama ni ya kujipamba. Yanatakiwa kuwa na uzani kaisi gani ili yatolewe zakaah na ni kipi kiasi chake?

Jibu: Maoni yenye nguvu ni kwamba mwanamke anatakiwa kuyatolea zakaah mapambo yake yakifikisha kile kiwango cha wajibu. Kiwango cha lazima ni gramu 85. Kama mwanamke anayo mapambo yasiyokuwa chini ya gramu 85 basi anatakiwa kuyatolea zakaah 2.5%. Kila mwaka anatakiwa kuhesabu thamani yake na kuyalipia 2.5%. Asizingatie ile bei ambayo ameyanunua, kwa sababu inaweza kupanda na pia inaweza kushuka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/133)
  • Imechapishwa: 07/05/2021