Kutoa Zakaat-ul-Fitwr zaidi kwa lengo la swadaqah

Swali: Je, inajuzu kuzidisha katika Zakaat-ul-Fitwr kwa nia ya kutoa swadaqah?

Jibu: Ndio, inafaa kufanya hivo. Yale yanayofanywa na baadhi ya watu kwa mfano wanatakiwa kutoa Zakaat-ul-Fitwr juu ya watu kumi ambapo wananunua mfuko mzima wa mchele ambao unaweza kuwafikia zaidi ya watu kumi. Anautoa mfuko huo kwa ajili yake na juu ya familia yake. Kufanya hivo inafaa ikiwa ana uhakika kuwa mfuko huo utatosha kile kiwango kinachowamujibikia. Hakuna ambacho ni wajibu isipokuwa kujua kile kiwango. Tukijua kuwa kiwango hicho kimefikiwa kwa mfuko huo, basi tutautoa wote kumpa fakiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/286)
  • Imechapishwa: 07/05/2021