Namna ya kuwanyamazisha wanaozungumza wakati wa Khutbah

Swali: Wakati Khutbah ya ijumaa inaendelea kunakuwepo watoto wanaosumbua watu. Je, wazinduliwe au waashiriwe tu?

Jibu: Wale walioko karibu nao wawaashirie kunyamaza. Ishara inatosha.

Swali: Je, imamu ampe kazi mtu mmoja ya kuwatazama?

Jibu: Inafaa kwa imamu kuzungumza na kuwaambia watu wawanyamazishe. Hapana vibaya. Inafaa kwa imamu, Khatwiyb, peke yake, kuzungumza kutokana na manufaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliongea katika baadhi ya Khutbah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22720/حكم-الاشارة-للاطفال-بالسكوت-وقت-الخطبة
  • Imechapishwa: 04/08/2023