Namna ya kutikisa kidole kwenye Tashahhud

Swali 328: Kidole kinatikiswa vipi ndani ya swalah katika Tashahhud?

Jibu: Kuna Hadiyth ya Waa-iyl bin Jariyr, ambaye amesimulia kuwa alimuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa amekaa chini kwenye Tashahhud katika swalah, akasema:

“Nikamuona akikitikisa huku akiomba kwacho.”

Hivi ndivo alivokuwa akitikisa[1]. Haina maana ya kutikisa chini na juu. Hakuna Hadiyth zilizosema hivo kabisa. Kuhusu kutikisa mtu anatikisa kikiwa mahali pake. Vilevile imesihi kutoka kwa Imaam Ahmad kwamba amesema:

“Akitikise sana.”

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-lini-mtu-ataanza-kutikisa-kidole-katika-tashahhud/

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 124
  • Imechapishwa: 29/07/2019