Swali: Ipi Sunnah kuhusiana na kutikisa kidole cha shahadah katika swalah. Ni mamoja katika Tashahhud au wakati wa kusoma “al- Faatihah” na kinachokuja baada yake?

Jibu: Wakati wa hali ya kisomo ni kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua. Hapa ni katika ile hali ya kusimama. Na atapokaa kwenye Tashahhud ataashiria kidole cha shahadah, atakunja kiganja chake [kama ngumi] na kuashiria kidole cha shahadah. Huu ni wakati wa kukaa Tashahhud. Itapofika wakati wa du´aa basi atakitikisa kidole chake kidogokidogo, wakati ataanza kusema:

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى

“Ee Allaah! Msifu…. ”

 Na wakati ataposema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابِ جهنم

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba ulinzi kutokamana na adabu ya Jahannam… ”

Wakati wa:

اللَّهُمَّ أَعِنِّي على ذِكْرِكَ

”Ee Allaah! Nisaidie kuweza kukukumbuka… ”

au du´aa yoyote ataashiria na kukitikisa kidogokidogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 29/07/2019