Swali: Nimejiliwa na mtu anayekunywa pombe. Nitangamane naye vipi?

Jibu: Akinywa anatakiwa kunasihiwa, abainishiwe na kuelekezwa katika kheri na asirudi. Asilaaniwe na asitukanywe. Asisaidiwe shaytwaan dhidi yake. Aombewe kwa Allaah amwongoze, amtengeneze na amtunuku tawbah. Muislamu ni nduguye muislamu ambapo anatakiwa kumpendea kheri. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoambiwa: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika Daws wameasi na wamekataa kusilimu.” Alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ee Allaah! Waongoze Daws na niletee nao.”

Muislamu anatakiwa kumwombea nduguye yaliyo ya kheri, amwombee kutubu tawbah ya kweli, asimfedheheshe na wala asimtukane. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwalaani baadhi ya watu ambao walitangaza shari yao dhidi ya waislamu kama vile Abu Jahl na wengineo. Alikuwa amekwishakata tama kuwaombea du´aa njema. Ikidhihiri shari yao juu ya waislamu basi hapo kuwaombwa dhidi yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21590/كيف-يكون-التعامل-مع-شارب-الخمر
  • Imechapishwa: 18/08/2022