Namna ya kupanga majeneza mengi yanayotaka kuswaliwa

Swali: Inatokea katika baadhi ya kumbi za kumswalia maiti ikiwa kuna majeneza mengi ya wanawake na wanaume wanatangulizwa mbele wanaume na wanakemea kwa ukali akitangulizwa mbele mwanamke. Je, ukemeaji huu una mashiko?

Jibu: Sunnah ni kuwatanguliza mbele wanaume. Hii ndio Sunnah wanaume ndio watangulizwa mbele karibu na imamu kisha baada ya hapo wanawake. Asimame katikati ya mwanamke usawa na vichwa vya wanaume ili apate kuwaswalia wote. Ikiwa ni mwanamme na mwanamke, basi mwanaume atangulizwe mbele karibu na imamu na mwanamke awe nyuma yake  katikati yake na usawa na kichwa cha mwanaume. Na ikiwa kuna watoto, ataanza mtoto wa kiume, afuatie mtoto wa kiume, halafu afuatie mtoto wa kike, kisha afuatie mtoto wa kike.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23554/حكم-تقديم-جناىز-الرجال-على-جناىز-النساء
  • Imechapishwa: 10/02/2024