Swali: Zakaah ya hisa inakuwa juu ya ile thamani rasmi ya hisa au thamani ya soko?

Jibu: Zakaah ya hisa na bidhaa nyenginezo inategemea na ile thamani ya soko. Ikiwa amenunua hisa kwa 1000 kisha ile hisa ikapanda 2000 katika kipindi ambacho imewajibika kuitolea zakaah, basi zakaah itayotolewa ni 2000. Kwa sababu kinachozingatiwa ni ile thamani ya kitu pindi umefika wakati wake wa kuitolea zakaah na si ile bei ya ununuzi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/197)