Swali: Ni ipi hukumu ikiwa watu wamepata khabari kwamba ni ´iyd baada ya jua kipinduka?

Jibu: Ikiwa wamepata khabari kwamba ni siku ya ´iyd baada ya jua kupondoka, basi wanatakiwa kufungua siku hiyo na waswali swalah ya ´iyd siku ya kufuata.

Kuhusu ´Iyd-ul-Adhwhaa, watatakiwa kuswali siku ya kufuata na wasichinje kabla ya swalah ya ´iyd. Kichinjwa kimeambatana na swalah. Maoni yaliyotangaa ya madhehebu yanasema watu wanatakiwa kuchinja ikiwa umemalizika muda wa swalah baada ya kupinduka kwa jua, lakini maoni ya kwanza ndio salama zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/229-230)
  • Imechapishwa: 08/05/2021