Swali: Niko na kiwango cha pesa cha mtu ambaye ni mynonge amekiweka kwangu nimchungie amana. Zimekwishazungukiwa na mwaka mzima. Je, inafaa kwangu kumtolea zakaah kutoka katika mali yangu binafsi kwa sababu pesa yake ni ndogo na mtu huyo ni fakiri?

Jibu: Zakaah ni miongoni mwa ´ibaadah kubwa na nguzo kubwa ya Uislamu. Haifai kufanya ´ibaadah yoyote isipokuwa kwa kuweka nia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika si venginevo kila kitendo kinategemea na nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.”[1]

Mambo yakishakuwa hivo ni kwamba haijuzu kumtolea zakaah mtu mwengine isipokuwa baada ya yeye kukuwakilisha. Ama pasi na uwakilishwaji ni jambo lisilofaa. Ukimtolea zakaah pasi na yeye kukuwakilisha, anakuwa hakuweka nia ya kuitoa. Utoaji ukifanyika pasi na manuizi hautosihi.

[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/308)
  • Imechapishwa: 08/05/2021