Swali: Mimi nawaona baadhi ya waswaliji pindi wanapoinuka kutoka katika Rukuu´ basi wananyanyua mikono yao kana kwamba wanaomba du´aa. Je, kitendo chao hichi kinaafikiana na Sunnah?

Jibu: Sunnah kwa mswaliji ni yeye anyanyue mikono yake usawa wa mabega yake au usawa wa masikio yake wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam, wakati wa Rukuu´ na wakati wa kuinuka kutoka katika Rukuu´, wakati wa kuinuka kutoka katika Tashahhud ya kwanza na kwenda katika Rak´ah ya tatu na huku matumbo ya vidole yanaelekea upande wa Qiblah. Hii ndio Sunnah iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/115)
  • Imechapishwa: 23/10/2021