Namna ya kufanya Tayammum II

Swali: Ni vipi vinatakiwa kupanguswa viganja vya mikono?

Jibu: Atafuta namna hii; kwa ndani na kwa nje yake. Hiki [kusugua nyuma ya kiganja cha kushoto] kwa hiki [kiganja cha kulia].

Swali: Baadhi ya wanazuoni wanasema kufaa kupiga kwenye godoro likiwa na vumbi.

Jibu: Hapana vibaya likiwa na vumbi kweli. Lakini bora na salama zaidi ni yeye akusudie mchanga ukiwepo na ukiwa karibu.

Swali: Kupangusa viganja vya mikono si inakuwa nje ya kiganja peke yake?

Jibu: Udhahiri ni kwa nje na kwa ndani. Kwa sababu neno ´mkono` limekusanya kwa ndani na kwa nje:

فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

”… panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Swali: Atavipuliza?

Jibu: Vikiwa na vumbi jingi la mchanga basi avipulize ili kuipunguza.

[1] 04:43

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23570/ما-كيفية-مسح-الكفين-في-التيمم
  • Imechapishwa: 14/02/2024