Tayammum kwa anayekhofia kumalizika muda wa swalah

Swali: Kuna dhana yake kubwa inamwambia kuwa kuna maji, lakini anakhofia kumalizika muda wa swalah.

Jibu: Aswali kwa Tayammum ikiwa hana maji:

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

“Mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni na mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akija kutoka msalani au mmewagusa wanawake kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi kwa juu panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[1]

Isipokuwa ikiwa kama mahali hapo ni karibu ayaendee maji. Katika hali hiyo haitojuzu kufanya Tayammum maadamu ni ndani ya wakati.

Swali: Je, akate swalah ikiwa maji yatakuja katikati ya swalah?

Jibu: Maoni ya karibu zaidi na usawa ni kwamba akate swalah na atawadhe. Hilo ni kutokana na kuenea kwa maneno Yake:

فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا

”… kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum… ”

Akipata maji na yakaletwa mbele yake aikate, atawadhe kisha airudie swalah.

[1] 04:43

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23569/هل-يجوز-التيمم-لمن-خاف-فوات-الوقت
  • Imechapishwa: 14/02/2024