Namna hii utajikwamua na pesa isiyokuwa ya halali

Swali: Inafaa kwa mtu ambaye yuko na mali isiyokubalika katika Shari´ah kuwapa nayo mafukara na kuchapisha vitabu na kaseti?

Jibu: Ndio. Ambaye yuko na pesa mbaya azitoe katika njia za kheri; kuwapa swadaqah mafukara au kuchapisha vitabu. Hapana neno.

Swali: Swadaqah hiyo inakubaliwa?

Jibu: Hapana, ni kwa njia ya kuitakasa dhimma yake na kupata baraka. Anapewa ujira kama swadaqah nzuri – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23135/حكم-التصرف-في-الاموال-غير-المشروعة
  • Imechapishwa: 09/11/2023