Nyama iliyochinjwa kwa jina la Masiyh

Swali: Je, inafaa kula nyama ya mnaswara ambaye nimemsikia akimchinja mnyama kwa jina la Masiyh?

Jibu: Allaah ameihalalisha ingawa anajua kuwa wanasema hivo. Muda wa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) amehalalisha, na isitoshe ni kichinjwa cha watu wa Kitabu, ni halali kula. Na ukiacha kwa ajili ya kuchukizwa au uchaji, inafaa kwako kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 10/11/2023