Swali: Elimu ambayo haimnufaishi mtu ni zile za kimazingira?

Jibu: Kila elimu ambayo hainufaishi inaingia ndani yake. Hata elimu ya Shari´ah ikiwa hainufaishi inakuwa ni hoja dhidi ya mwenye nayo. Tunamuomba Allaah usalama. Ikiwa mwenye nayo haitendei kazi inakuwa ni hoja dhidi yake.

Swali: Elimu za kilimwengu si zinaingia katika zile elimu zisizonufaisha?

Jibu: Hapana. Elimu za kimazingira zinaweza kunufaisha. Elimu ya fundi seremala inamnufaisha mwenye nayo. Elimu ya mhunzi inamnufaisha mwenye nayo. Elimu ya udereva inamnufaisha mwenye nayo. Hata hivyo baadhi ya watu wanayo elimu ya Shari´ah, kama mfano wa mayahudi na elimu nyenginezo mbovu, zisizowanufaisha. Elimu hiyo ni hoja dhidi yao siku ya Qiyaamah kuwapelekea Motoni. Tunamuomba Allaah usalama.

Swali: Kwa hivyo manufaa yanayokusudiwa ni duniani na Aakhirah?

Jibu: Inakusanya yote mawili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23134/ما-هو-العلم-الذي-لا-ينفع
  • Imechapishwa: 09/11/2023