Namna hii ndivyo mtu anaingia katika utumwa wa shaytwaan

Swali: Ni ipi hukumu ya msemo wa mtenda maasi pindi anapokemewa:

“Mimi niko huru kufania nikitakacho?”

Jibu: Hili ni kosa. Mtu huyu hayuko huru katika kumuasi Allaah. Tunamwambia kuwa endapo atamuasi Mola wake basi ametoka katika utumwa wa Allaah – ambao anadai – na badala yake ameenda katika utumwa wa shaytwaan na matamanio.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/81)
  • Imechapishwa: 06/06/2017