Ni ipi hukumu ya kutumia neno “bwana” kwa asiyekuwa Allaah?

Swali: Ni ipi hukumu ya tamko “bwana” –  السيد – kwa asiyekuwa Allaah?

Jibu: Kutumia neno ´bwana` kwa asiyekuwa Allaah ikiwa anakusudia ile maana yake ambayo ni bwana asiyefungamanishwa itakuwa haijuzu. Ikiwa anakusudia heshima tu ilihali yule mwenye kuitwa hivo anastahiki kuitwa hivo hakuna neno. Lakini hata hivyo asiseme “bwana”. Badala yake aseme “ee bwana” au mfano wa hivo. Hakuna neno vilevile ikiwa hakusudii heshima isipokuwa analitumia tu kama jina.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/109)
  • Imechapishwa: 06/06/2017