Swali: Ni ipi hukumu ya msemo wa baadhi ya watu:
“Mimi niko huru?”
Jibu: Maneno hayo yakisema mtu ambaye kweli yuko huru na akawa anakusudia kwamba yuko huru na utumwa wa viumbe, hilo ni kweli kwamba yuko huru na utumwa viumbe. Lakini ikiwa anakusudia kuwa yuko huru kutokamana na kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall), basi amekosea katika kufahamu uja. Isitoshe ni kuwa hakufahamu maana ya uhuru. Uja kwa asiyekuwa Allaah ndio utumwa. Ama mtu kuwa mja kwa Mola wake (´Azza wa Jall) ndio uhuru wenyewe. Asipomnyenyekea Allaah basi atamnyenyekea asiyekuwa Allaah. Katika hali hii anakuwa ni mwenye kuidanganya nafsi yake pindi anaposema kuwa yuko huru na huku akimaanisha kuwa hana uwajibu wa kumtii Allaah.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/81)
- Imechapishwa: 06/06/2017
Swali: Ni ipi hukumu ya msemo wa baadhi ya watu:
“Mimi niko huru?”
Jibu: Maneno hayo yakisema mtu ambaye kweli yuko huru na akawa anakusudia kwamba yuko huru na utumwa wa viumbe, hilo ni kweli kwamba yuko huru na utumwa viumbe. Lakini ikiwa anakusudia kuwa yuko huru kutokamana na kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall), basi amekosea katika kufahamu uja. Isitoshe ni kuwa hakufahamu maana ya uhuru. Uja kwa asiyekuwa Allaah ndio utumwa. Ama mtu kuwa mja kwa Mola wake (´Azza wa Jall) ndio uhuru wenyewe. Asipomnyenyekea Allaah basi atamnyenyekea asiyekuwa Allaah. Katika hali hii anakuwa ni mwenye kuidanganya nafsi yake pindi anaposema kuwa yuko huru na huku akimaanisha kuwa hana uwajibu wa kumtii Allaah.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (03/81)
Imechapishwa: 06/06/2017
https://firqatunnajia.com/mimi-niko-huru-kufanya-nitakacho/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)