Namna hii ndivyo Allaah alimuumba Aadam kwa sura Yake

Swali: Ni ipi maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah alimuumba Aadam kwa sura Yake.”?

Jibu: Kwa udhahiri wake. Dhamiri ya “kwa sura Yake” inarejea kwa Allaah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ سَمِيعًا بَصِيرًا

“Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na tone la manii iliyochanganyika ili Tumjaribu, hivyo tukamjaalia mwenye kusikia na kuona.” (76:02)

Allaah alimuumba Aadam kwa sura Yake kutokamana na kwamba Aadam pia ana usikizi, uoni na sifa nyenginezo. Sifa hizi zinapatikana kwa Allaah na kwa viumbe vilevile. Lakini hata hivyo hakuna ufananizi wowote kati ya hizo mbili. Sifa za Muumba hazifanani na sifa za viumbe hata kama zinashirikiana katika maana na  asli. Zinatofautiana:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (42:11)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-06_0.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2020