Swali: Ni wajibu kwa muislamu kuchukia kufuru ya kafiri au hata kafiri mwenyewe?

Jibu: Ni wajibu kwake kumchukia kafiri na kufuru; yote mawili. Kufuru inatakiwa kuchukiwa na kafiri mwenyewe kwa sababu ni adui wa Allaah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ يُخْرِجُونَ الرَّسُولَ وَإِيَّاكُمْ ۙ أَن تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ رَبِّكُمْ

“Enyi mlioamini! Msimchukue adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki mkiwapelekea mapenzi na hali wamekwishakanusha haki iliyokujieni. Wanamtoa kwa kumfukuza Mtume pamoja na nyinyi kwa vile mmemuamini Allaah Mola wenu.” (60:01)

Tunawachukia makafiri na tunachukia dini yao. Asiyewachukia makafiri hana kupenda na kuchukia kwa ajili ya Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-08-06_0.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2020