Swali: Ni kipi kinachopanguswa kwenye soksi? Je, ni lazima kupangusa sehemu ya juu yote ya soksi au mtu apanguse sehemu maalum tu?

Jibu: Ni kama zinavyopanguswa soksi za ngozi; kuanzia mwanzoni mwa vidole vya miguuni hadi kwenye tibia. Sehemu ya juu ya soksi za kawaida na sehemu ya juu ya soksi za ngozi. Atapitisha vidole vyake hali ya kuwa amevilowesha maji kuanzia mwazoni mwa vidole vya miguu hadi kwenye tibia mara moja. Sehemu ya nyayo haitopanguswa wala sehemu yake ya kando.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 12/07/2024