Swali: Je, mtu aende katika vikao vya Ahl-ul-Ahwaa´ na kuhudhuria mihadhara yao na kuwatolea Salaam?

Jibu: Huyu mara nyingi akienda hugeuka akawa Hizbiy. Ima anakuwa ni katika Tabliygh, pote katika Suufiyyah au Raafidhwiyyah, Jahmiyyah au Mu´tazilah. Ni lazima iwe hivi kwa kuwa aina ya watu hawa hupewa adhabu na Allaah. Kwa kuwa wameenda kinyume na uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maelekezo yake. Kadhalika wameenda kinyume na uongofu wa Salaf. Watu hawa mara nyingi hupotea na huwa pamoja na makundi ya shari.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26890
  • Imechapishwa: 20/05/2015