Swali: Leo inatosheleza kwa mtu Salafiy kujua haki na batili au ni wajibu kwake vilevile kuwapiga Radd Ahl-ul-Ahwaa´ na hayo ndio mambo yataipambanua Da´wah yake?

Jibu: Wajibu kwa mtu Salafiy ni yeye kuijua haki, alinganie kwayo na awabainishie nayo watu. Ni juu yake kusimama na wajibu huu. Kunahitajia vilevile kutoka kwake, kutokana na elimu hii [alionayo] na ulinganio huu aiangushe batili. Kwa kuwa Qur-aan Tukufu inaibainisha haki na kuiangusha batili kwa wakati mmoja. Kwa ajili hii ndio maana ikaitwa “al-Mathaaniy” kwa sababu inataja kheri na shari, inaita katika kheri na inatahadharisha na shari, inawataja waumini na wanafiki. Vilevile inataja shari walizonazo makafiri, mayahudi na manaswara.

Uislamu umesimama juu ya nguzo hizi ambazo tumezifafanua kama jinsi umesimama pia juu ya Jihaad, kuamrisha mema na kutahadharisha maovu. Haya ndio Uislamu umesimama juu yake. Uislamu haunyooki isipokuwa kwa kusimamisha haki, kuiweka wazi na kuibainisha na wakati huo huo kuiangusha batili na kubainishia watu ubaya wake na kutahadharisha nayo na watu wake. Uislamu unasimama kwa haya.

Da´wah yoyote isiyosimama kwa wajibu huu ni Da´wah iliyopinda na ni maiti. Da´wah haiwi hai isipokuwa pale ambapo inakuwa ni yenye kunyanyua bendera ya haki na wakati huo huo kuiangusha batili. Huu ndio uhakika wa mambo. Kwa ajili hii ndio maana Amesema (Ta´ala):

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa [mfano] kwa watu; mnaamrisha mema na mnakataza maovu.” (03:110)

Asiyeraddi batili vipi anaamrisha mema na kukataza maovu? Ni kama mfano wa Jamaa´at-ut-Tabliygh wanasema wanaamrisha mema ilihali hawaamrishi mema. Hawawafundishi watu Tawhiyd. Kadhalika hawawafundishi watu sifa ya Swalah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ilihali wanadai kuwa wanaamrisha mema. Ukweli wa mambo ni kwamba hawakuamrisha mema na wala hawakukataza maovu. Tunamuomba Allaah afya. Ni ipi tofauti kati yako wewe na wapotevu hawa ikiwa huipigi vita Bid´ah, upotevu na kuwaraddi watu wapotevu? Iko wapi tofauti kati yako wewe na wao?

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26890
  • Imechapishwa: 20/05/2015