Mzazi anamzuia mwanawe kusoma elimu ya dini

Swali: Ni ipi hukumu ya kutafuta elimu pamoja na kuzingatia kwamba baba yangu amenikatalia kwenda chuoni kwa sababu ya kunihitajia kwake. Nina ndugu yangu mwingine ambaye anafunza katika kitongoji ambacho anaishi baba yangu.

Jibu: Naona kuwa baba yake amekosea kumkatalia mtoto wake kuingia chuoni. Kwa sababu sisi tuko katika wakati ambapo mtu hawezi kunufaika wala kuwanufaisha wengine isipokuwa akipata vyeti. Ushauri wangu kwa baba huyu awaache watoto wake wasome kwa kiasi na vile ilivyo hali yao kutoka katika vyuo vikuu, masomo ya kawaida na mengineyo. Inahusiana na vile vyuo vilivyo na elimu yenye manufaa. Ikiwa anahitajia mfanya kazi basi anaweza – ikiwa kama Allaah amemtajirisha – kuleta mfanya kazi ambaye ataishi hapo kwake na kumkidhia haja zake. Ama kumzuilia mtoto wake na elimu kwa sababu eti anamuhitajia ni kitu kilicho na aina fulani ya madhara kwa mtoto.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (48) http://binothaimeen.net/content/1093
  • Imechapishwa: 06/04/2019