Myemeni ameingia Ihraam kutokea Jeddah

Swali: Kuna mtu anataka kufanya ´Umrah na mara nyingi anasafiri kwa ndege kuja huku kutokea Yemen. Hata kama atakipita kituo ataanza kwanza kuingia katika Ihraam Jeddah kwa sababu anaishi hapo. Je, kuna kinachomlazimu?

Jibu: Ndio. Ameacha Ihraam kutoka kituoni. Ni lazima atoe fidia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (22) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-26-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 27/03/2020