Mwombaji anayepasa na asiyepasa kuitikiwa maombi yake

Swali: Mwenye kumuomba mwengine kwa jina la Allaah na akaomba kinga kutokana na fulani na asipewe anachoomba.

Jibu: Asiombe kwa jina la Allaah. Lakini anayeomba kwa jina la Allaah na wakati huohuo anastahiki anapaswa kupewa. Anayeomba kinga kwa Allaah anapaswa kupewa ijapo kidogo. Hapa ni pale ambapo anastahiki. Lakini kwa mfano anaomba kupewa zakaah na si katika wale watu wanaostahiki kupewa zakaah au akaomba kinga kwa Allaah asisimamishiwe adhabu ya Kishari´ah, hatakiwi kupewa. Hili ni katika yale mambo yanayowezekana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23230/هل-تلزم-اجابة-من-سال-او-استعاذ-بالله
  • Imechapishwa: 07/12/2023