Swali: Maneno ya Shaykh-ul-Islaam kwamba fundi wa mikono na mwokoaji watakusanya swalah wakikhofia juu ya mali zao.

Jibu: Haya yamesemwa na kikosi cha wanazuoni na kwamba hizi ni kazi zenye ugumu ili asije kuwatia uzito ummah wake, kama alivosema Ibn ´Abbaas. Kwa sababu akiacha kufanya hivo inaweza kuwa vigumu kwake na ikaharibika mali yake. Wakati mwingine pengine wakalazimika kufanya hivo. Lakini inatakiwa kwa muumini kujihadhari kukusanya swalah isipokuwa kunapokuwa sababu ya wazi. Lililo la wajibu ni kuswali kila swalah ndani ya wakati wake, kwa sababu Allaah amepanga nyakati na akalazimisha isipokuwa tu safarini, wakati wa mvua au wakati wa ugonjwa. Vinginevyo wakati mtu anapokuwa na afya njema anapaswa kutahadhari juu ya hilo isipokuwa kunapokuwa kuna sababu inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23675/حكم-جمع-الصانع-والخباز-للصلاة
  • Imechapishwa: 30/03/2024