Je, makafiri watamuona Allaah katika uwanja wa mkusanyiko?

Swali: Je, makafiri  watamuona Mola wao katika uwanja wa mkusanyiko?

Jibu: Hawatomuona isipokuwa tu waumini:

كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ

“Sivyo hivyo! Hakika wao Siku hiyo bila shaka watazuiwa wasimuone Mola wao.”[1]

Swali: Hadiyth isemayo:

“Hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa Mola Wake atamzungumzisha.”?

Jibu: Mazungumzo sio kuona.

[1] 83:15

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23679/هل-يرى-الكفار-ربهم-في-الموقف
  • Imechapishwa: 30/03/2024