Mwenye madhara ya sukari afunge au asifunge?

Swali: Ikiwa mtu ana maradhi ya kisukari na anadunga sindano za kawaida na sio zile za kuingiza chakula na afya yake si mbaya sana bora kwake kufunga au kuacha kufunga?

Jibu: Hili linategemea ile kanuni tuliyotaja; je, swawm inamtia uzito na inamdhuru? Ikiwa swawm inamtia uzito basi itakuwa imechukizwa kwake kufunga. Ikiwa inamdhuru basi itakuwa ni haramu kwake kufunga. Madaktari wakisema kwamba endapo atatumia sindano mara kwa mara basi sukari yake inamuua basi katika hali hii ni wajibu kwake kuacha kufunga. Himdi zote anastahiki Allaah ambaye anapenda zitendewe kazi ruhusa zake kama ambavyo anachukia kutendewa kazi maasi yake. Bali kuacha kufunga katika hali ya madhara ni lazima na sio ruhusa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (33) http://binothaimeen.net/content/740
  • Imechapishwa: 20/11/2017