Mwenye kuswali swalah ya ijumaa tu ni afiri – asiyeswali katika jamaa´ah ni mnafiki

Swali: Kuna ambao hawaswali swalah za faradhi na hawahudhurii isipokuwa swalah ya ijumaa tu. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Ikiwa anaacha swalah za faradhi na haswali isipokuwa swalah ya ijumaa tu, huyu ni kafiri. Yule anayeswali swalah ya ijumaa pamoja na jamaa´ah na anaacha kuswali swalah zingine pamoja na jamaa´ah, huyu ni mnafiki. Yule mwenye kuacha kuswali ya swalah ya mkusanyiko ni mnafiki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemsifu kuwa ni mnafiki:

”Swalah nzito kwa wanafiki ni swalah ya ´Ishaa na Fajr.”

´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Hatukuwa tukiona mwenye kuiacha – yaani swalah ya mkunsanyiko – isipokuwa mnafiki tu unayejulikana unafiki wake.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqa-08-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 23/04/2015