Swali: Tunapenda utunasihi leo wakati Anaashiyd kati ya vijana wa kidini zimeendelea sana, picha na michezo ya vijana katika barnamiji za jumla.

Jibu: Yote haya ni Bid´ah. Hayana asli katika dini. Anaashiyd ni aina ya nyimbo na pumbao. Ni alama ya Hizbiyyuun. Ninasema haya wazi wazi kabisa: ni alama ya Hizbiyyuun! Sio alama ya Ahl-us-Sunah. Au ni alama ya Suufiyyuun. Wanaabudu kwazo. Allaah ametuamrisha kumuabudu kwa Qur-aan na tuzingatie Qur-aan na kusikiliza Qur-aan. Ndio njia ya manufaa. Hakuna kinachotufikisha kwa Allaah isipokuwa Qur-aan iliyo na enzi na tukufu imetubainishia. Vipi tuiache na kwenda katika Anaashiyd, Twitter na mambo kama haya? Hakuna shaka ya kwamba jamii hii ndio yote ambayo Waislamu wamebaki nayo. Kuna Qiblah, Ka´bah tukufu na msikiti Mtakatifu na msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni lazima nchi hii iwe tofauti katika mfumo wake. Iwe ni mfano na kiigizo kwa ulimwengu mzima wa Kiislamu. Ni lazima watu watahadhari na mambo haya ili wasitumbukie ndani yake, kuwaathiri vijana wao, wanawake na wajinga.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/liqo-01-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 23/04/2015