64. Mwenye kujilipua na kujiua haamini makadirio ya Allaah

Leo hii mnasikia sana yale yanayoitwa ´kujilipua na kujiua` na kwamba ni jambo limeenea kati ya watu wenye dini zengine. Sababu yake ni nini? Sababu yake ni kutoamini mipango na makadirio. Pindi mmoja wao anapohisi dhiki anajilipua. Kwa sababu haamini mipango na makadirio. Hasemi kuwa ni jambo alilokadiriwa na kuandikiwa na akaamini kuwa faraja iko karibu na akamdhania Allaah vyema:

فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا

“Hakika pamoja na kila gumu kuna mepesi.” (94:05)

أَلَا إِنَّ نَصْرَ اللَّـهِ قَرِيبٌ

“Tanabahi! Hakika nusura ya Allaah iko karibu.” (02:214)

Ambaye anajilipua na kujiua haamini mipango na makadirio. Hawezi kustahamili matatizo na misiba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 151
  • Imechapishwa: 12/01/2024