Mwenye kufanya dhambi kubwa haina maana kwamba anaona kuwa ni halali

Swali: Maneno ya Ibn ´Abbaas aliposema:

“Kufuru ilio chini ya kufuru.”

Anakusudia nini?

Jibu: Maana yake ni kule kuhukumu kinyume na yale aliyoteremsha Allaah muda wa kuwa mtu hajahalalisha.

Swali: Hata kama ataiba na kuzini?

Jibu: Vivyo hivyo.

Swali: Kitendo chenyewe hakifahamishi kuwa mtu amehalalisha?

Ibn Baaz: Mtu akizini anahukumiwa kuwa amehalalisha?

Muulizaji: Hapana.

Ibn Baaz: Kwa hiyo ni kipi chenye kumfanya akakufuru? Akizini, akafanya liwati au akanywa pombe tutasema kuwa amekufuru?

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 21/07/2019