Mwenye kuchelewa kusindikiza jeneza anapewa thawabu?

Swali: Mtu akichelewa kulisindikiza jeneza kwa sababu ya msongamano, swalah ya Sunnah, swalah ya faradhi au sababu nyingine na matokeo yake asiliandame jeneza lakini amewahi kuswali swalah ya jeneza kabla ya kuzikwa – anazingatiwa kuwa amelisindikiza na anapata ujira wa kusindikiza?

Jibu: Mwenye kuchelewa kwa ajili ya swalah ya Sunnah na kusindikiza jeneza kukampita hapewi thawabu za kulisindikiza. Mtu anaweza kuchelewesha swalah ya Sunnah na kuiswala baada ya mazishi.

Anayechelewa kwa sababu ya udhuru kama msongamano wa watu au kukamilisha faradhi na alikuwa amekuja kwa ajili pia ya kusindikiza jeneza dhahiri ni kuwa anapewa thawabu. Kwa kuwa amenuia na amefanya kile anachoweza. Mwenye kunuia na kufanya vile anavyoweza anaweza kuandikiwa thawabu kamilifu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يُهَاجِرْ فِي سَبِيلِ اللّهِ يَجِدْ فِي الأَرْضِ مُرَاغَمًا كَثِيرًا وَسَعَةً وَمَن يَخْرُجْ مِن بَيْتِهِ مُهَاجِرًا إِلَى اللّهِ وَرَسُولِهِ ثُمَّ يُدْرِكْهُ الْمَوْتُ فَقَدْ وَقَعَ أَجْرُهُ عَلى اللّهِ وَكَانَ اللّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Anayehajiri katika njia ya Allaah atapata katika ardhi mahali pengi pa kukimbilia na wasaa. Na atakayetoka nyumbani kwake hali ya kuwa ni mwenye kuhajiri kwa ajili ya Allaah na Mtume Wake, halafu mauti yakamfikia [njiani], basi ujira wake umehakikika kwa Allaah. Na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

[1] 4:100

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/169-170)
  • Imechapishwa: 01/09/2021