Swali: Kuna ambaye alimuota mtu aliyefariki kwa muda. Ndotoni alimwamrisha kumtoa ndani ya kaburi na kumjengea kuba na akawa amefanya hivo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Ni haramu. Ndoto ikiwa inaenda kinyume na Shari´ah ni batili na ni kutoka kwa shaytwaan. Haijuzu kutekeleza hilo kwa hali yoyote ile. Hukumu za Kishari´ah hazibadiliki kwa ndoto. Lililo la wajibu saa hii ni kubomoa kuba hili walilojenga na kumrudisha maiti katika makaburi ya waislamu.

Nasaha zangu kwa watu hawa na mfano wao wazipime ndogo zao kwa Quraan na Sunnah. Kila kinachoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah ni chenye kutupiliwa mbali na hakikubaliwi. Haijuzu kwa mtu kuijenga dini yake juu ya ndoto hizi za uongo. Shaytwaan aliapa kwa nguvu za Allaah (´Azza wa Jall) ya kwamba atawapoteza watu isipkuwa waja wa Allaah wakweli. Yule ambaye ni mja wa kweli wa Allaah basi atasalimika kutokamana na upotoshaji na shari za shaytwaan. Wengine wote shaytwaan huziharibu ´ibaadah zao, ´Aqiydah zao, fikira zao na matendo yao mengine. Mtu anatakiwa achunge sana. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمْ عَدُوٌّ فَاتَّخِذُوهُ عَدُوًّا إِنَّمَا يَدْعُو حِزْبَهُ لِيَكُونُوا مِنْ أَصْحَابِ السَّعِيرِ

“Hakika shaytwaan kwenu ni adui, hivyo basi mchukulieni kama adui. Hakika anaitia kikosi chake ili wawe miongoni mwa watu wa Motoni.”[1]

[1] 35:6

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/208)
  • Imechapishwa: 01/09/2021