Swali: Vipi ikiwa mtu yuko na janaba akatawadha na kukaa msikitini?
Jibu: Maoni sahihi ni kwamba asiketi mpaka kwanza akoge. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mimi siuhalalishi msikiti kwa mwenye hedhi na mwenye janaba.”
Imepokelewa kwamba wako baadhi ya Maswahabah walikuwa wakiketi hali ya kuwa na janaba. Pengine hawakufikiwa na Hadiyth hiyo. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ غَفُورًا
”.. na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini… ”[1]
Bi maana hali ya kuwa anapita tu msikitini.
[1] 04:43
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22816/حكم-جلوس-الجنب-في-المسجد
- Imechapishwa: 26/08/2023