Madhambi yanayosamehewa ni yale madogo

Swali: Kusamehewa madhambi ni jambo maalum kwa yale madhambi madogomadogo?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا

“Mkijiepusha madhambi makubwa mnayokatazwa Tutakufutieni madhambi yenu madogo na Tutakuingizeni katika mahali patukufu.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah tano, ijumaa moja mpaka nyingine na Ramadhaan mpaka Ramadhaan nyingine ni vyenye kufuta yaliyo kati yake midhali mtu atajiepusha na madhambi makubwa.”[2]

[1] 04:31

[2] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (994)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22821/هل-تكفير-السيىات-يخص-الصغاىر-فقط
  • Imechapishwa: 26/08/2023