Mwenye janaba kutawadha kabla ya kulala

Swali: Vipi kuhusu waliosema kuwa ni lazima kwa mwenye janaba kutawadha kabla ya kulala?

Jibu: Maneno mazuri, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia ´Umar:

”Tawadha kisha ndio ulale.”

Alimwamrisha kutawadha. Udhahiri ni uwajibu.

Swali: Je, anapata dhambi akilala bila ya kutawadha?

Jibu: Kunakhofiwa juu yake.

Swali: Vipi itafasiriwa Hadiyth isemayo:

”Alikuwa akipata janaba kisha analala na wala hagusi maji.”?

Jibu: Hadiyth hii ina kasoro. Ikiwa imesihi basi kinachokusudiwa kwa `maji` ni josho la janaba. Hata hivyo ni Hadiyth yenye kasoro na dhaifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23970/حكم-الوضوء-للجنب-قبل-النوم
  • Imechapishwa: 08/08/2024