Swali: Je, inafaa kwa mwanaume kuzifunga nywele zake?

Jibu: Ndio, hapana vibaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizifunga mpaka kwenye mabega. Hakuna makatazo. Sijui makazo juu yake. Isipokuwa ikiwa mtu anatambulika kuwa anafanya hivo kwa ajili ya kuwatega wanawake na amekusudia maovu. Katika hali hiyo atakatazwa. ´Umar alipofikiwa na khabari kwamba Naswr bin al-Hajjaaj anawatega wanawake akamwamrisha kukinyoa kichwa chake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24104/هل-يجوز-للرجل-ان-يضفر-راسه
  • Imechapishwa: 29/08/2024