Mwanaume kuswali katikati ya wanawake msikiti wa Makkah

Swali: Baadhi ya wanaume huswali katikati ya wanawake Haram. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haitakikani.. lakini akiwa ni mwanaume mmoja na hana mwanaume mwenzake haisihi swalah yake… ili kusitokee fitina kwa pande zote.

Swali: Je, anayeona kuwa ni sahihi swalah ya mwanaume mmoja anayeswali nyuma ya wanawake anahitaji kutoa dalili? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya safu mbaya zaidi kwa wanawake ni zile za mbelembele.

Jibu: Ikiwa ni mwanaume mmoja pekee anayeswali peke yake nyuma ya wanawake, swalah yake si sahihi. Ili swala hiyo iwe sahihi, wanahitaji kuwa wanaume wasiopungua wawili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24920/حكم-صلاة-الرجال-في-الحرم-بين-النساء
  • Imechapishwa: 04/01/2025