Swalah ya wanaume walioswali nyuma ya wanawake

Swali: Wanawake kusimama mbele ya safu za wanaume khaswa katika Haram mbili?

Jibu: Wanawake wanapaswa kusimama kwa pembeni. Katika msikiti wa Makkah na Madiynah wanatakiwa kuwepo sehemu ya kando ili wanaume wasiwe nyuma yao.

Swali: Je, mwanaume anaweza kusimama nyuma ya mwanamke ikiwa hapati nafasi nyingine?

Jibu: Haitakikani kwa mwanaume kusimama nyuma ya mwanamke, ingawa swalah yake ni sahihi. Hata hivyo haitakikani kufanya hivo. Kinachotakiwa ni kufuata Sunnah na kuepuka kuswali nyuma ya wanawake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24919/حكم-تقدم-النساء-على-صفوف-الرجال
  • Imechapishwa: 04/01/2025