Inafaa kumvuta mswaliji kutoka katika safu?

Swali: Je, inaruhusiwa kumvuta mtu kutoka safu ya kwanza?

Jibu: Usimvute mtu. Hadiyth inayozungumzia jambo hili ni dhaifu. Usimvute yeyote. Badala yake tafuta nafasi nyingine, subiri mpaka aje mtu au unaweza kupanga safu na imamu. Ikiwa swalah itakupita, basi unaweza kuswali peke yako.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24921/ما-يفعل-من-لم-يجد-فرجة-في-صلاة-الجماعة
  • Imechapishwa: 04/01/2025