Ni wajibu kwa imamu kuwazindua maamuma kusawazisha na kuziba pengo za safu

Swali: Je, kusawazisha safu wakati wa swalah ni wajibu?

Jibu: Ndio udhahiri. Imamu anapaswa kuwaamrisha waumini kusawazisha safu zao kama sehemu ya kuamrisha mema na kukataza mabaya. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaamrisha na kuwahimiza.

Swali: Vipi ikiwa safu tayari iko sawa?

Jibu: Haijalishi kitu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema ili wazinduke:

“Sawaisheni safu zenu.”

Swali: Je, ni lazima kugusana miguu?

Jibu: Ni lazima kuziba pengo zilizopo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24922/هل-الامر-تسوية-الصفوف-واجب-على-الامام
  • Imechapishwa: 04/01/2025