Swali: Je, inajuzu kwa bibi harusi kuvaa gauni la harusi kwenye usiku wa harusi yake ikiwa anajua kama kufanya hivyo ni kujifananisha na makafiri?

Jibu: Mwanamke anaweza kuvaa nguo nyeupe kwa sharti zisifanane na za wanaume. Ama kuhusiana na kwamba anajifananisha na makafiri, kujifananisha huku kumekatika leo. Wanawake wa Kiislamu wote leo wanazivaa kanzu hizi wakati wa kuolewa. Hukumu inatokana na sababu. Ikiwa kujifananisha kumesimama na kanzu imekuwa ni jambo la kawaida kati ya Waislamu na makafiri, hukumu inasimama. Tofauti moja ni kama nguo yenyewe kwa dhati yake ni haramu. Kwa hali hii itakuwa ni haramu bila ya kujali nini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: www.sahab.net
  • Imechapishwa: 21/09/2020