Swali: Ni ipi hukumu kwa bibi harusi akivaa mavazi meupe usiku wa harusi?

Jibu: Hakuna neno katika hilo kwa sababu kila tukio lina vazi lake, isipokuwa ikiwa itakuwa na maana ya kuwaiga makafiri au wanawake waasi, kwa kuwa hili ni jambo jingine sawa ikiwa ni nguo nyeupe, nyekundu au nyeusi. Ama kuhusiana na yeye kuwa na nguo khaswa nyeupe katika sherehe wakati wa usiku wa harusi na hakukusudia kujikurubisha kwa Allaah kwa tendo hilo, hivyo hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaail Nisaaiyyah (108-109)
  • Imechapishwa: 21/09/2020