Mke anatoka bila ya idhini ya mume wake

Swali: Ni ipi hukumu mwanamke kutoka nyumbani bila ya idhini ya mume wake?

Jibu: Ikiwa mume yuko, hatakiwi kutoka bila ya idhini yake.

Ikiwa hayupo, anaweza kutoka maadamu hajamkataza.

Swali: Je, anaweza kuwaomba idhini wazazi wake ya kwenda nje ikiwa mume hayupo?

Jibu: Kanuni ni kama tulivyosema ya kwamba anaweza kutoka maadamu mume wake hajamkataza. Ikiwa mume kabla ya safari yake alimwambia asitoke nyumbani au asiende sehemu maalum, asitoke hata kama wazazi wake watamuacha atoke. Ni mume ndio mwenye uamuzi juu yake na sio wazazi wake.

Swali: Mume akimwambia asitoke kabla ya kumuuliza, je, anaweza hivyo kuwaomba idhini wazazi wake?

Jibu: Hawachukui sehemu yake maadamu [mume] hajawaachia suala lake.

Check Also

Peleka mahakamani

Swali: Mimi nina dada anayegombana na mume wake mwenye madhehebu na mfumo wa Suufiyyah. Anampiga, …